Logifem, ni makazi ya wanawake walio katika ugumu

Kama unapitia ugumu na unatafuta makazi na usaidizi ili kuishi, usisite kutupigia simu katika nambari 514-939-3172.

Logifem ni nini?

Logifem hutoa makazi na usaidizi kwa wanawake walio na wasiokuwa na watoto jijini Montreal.

Makazi yetu makuu yanayo vyumba 14 vya wanawake na vyumba vikubwa zaidi 6 vya kuwahifadhi wanawake na watoto. Kunazo pia bafu za kutumiwa kwa pamoja na sehemu nyinginezo. Kipindi kirefu zaidi wanachoweza kuishi hapo ni mwaka mmoja.

Tunazo pia nyumba za ghorofa za mpito 13, sita zimehifadhiwa kwa ajili ya akina mama wasiokuwa na waume. Kipindi kirefu zaidi cha kukaa hapo ni miaka mitatu. Wanawake hulipia 25% ya mapato yao kama ada ya nyumba na lazima wawe na mradi wa kutangamana upya kijamii, ukiwemo ule wa kitaalamu au ule wa kurudi shuleni. Kwa kawaida unahitajika kupitia makazi ya kwanza ili kufikia yale ya pili ya nyumba ya ghorofa.

Ni kwa ajili ya nani?

Logifem huwakubali wanawake wote haijalishi ugumu wao, cheo chao, asili yao au lugha wanayozungumza. Hata hivyo, lazima watimize mpangilio ufuatao:

  • Wawe na umri wa kati ya miaka 18 na 65.
  • Waweze kimwili kupanda vidaraja hadi kwenye ghorofa ya tatu na kutekeleza kazi mbalimbali zinazopewa wakazi kila wiki: kuosha vyombo, kuosha mojawapo ya bafu, nk.
  • Waweze kulipia mchango wa kila mwezi unaokidhi vyakula vyao vyote na uwezo wao wa kufikia kiosha vyombo, kikaushaji, televisheni na kompyuta:
    • 400 $ kwa chumba kimoja
    • 50 $ kwa kila mtoto aliye na umri wa miezi sita au zaidi
    • (Kunao uwezekano wa kujadiliana mpangilio wa malipo kama una matatizo ya kifedha ya muda, tafadhali wasiliana na wafanyikazi wa mapokezi ili kuzungumzia hali yako).
  • Endapo utakuwa na tatizo la uzoefu wa matumizi ya dawa za kulevya au pombe, kuwa na ufuatilizi / tiba.
  • Meza dawa zozote kama ulivyoshauriwa (dawa inawekwa kwenye ofisi ya shughuli mbalimbali).Kuwa radhi kufuatiliwa na mfanyikazi wa saikolojia ya jamii.
  • Jitolee kuheshimu sheria za nyumba.
  • Kuwa na watoto wenye umri wa 12 au wachanga zaidi.

Tunajaribu kuwasiliana mambo muhimu na wanawake wakazi licha ya lugha yao wanayozungumza, tunaweza kuwaita wakalimani kama inavyohitajika. Hata hivyo, tunaweza tu kuahidi huduma katika Kifaransa na Kiingereza. Baadhi ya wazungumzaji wetu huzungumza lugha nyingine (Krioli, Kiarabu, Kihispaniola, Kiitaliano, Kilingala).

Tunasaidia vipi?

Logifem inaweza kukusaidia kama uko katika hali ngumu kwa kukupatia sehemu salama ya kuishi, chumba cha siri, vyakula mara tatu kwa siku na vitafunio mara tatu, chumba cha kuoshea nguo na ufikivu wa intaneti.Zaidi ya kuitikia mahitaji yako ya lazima, Logifem inatoa ufuatiliaji wa saikolojia ya jamii kwa wanawake wote wa kazi. Pindi unapowasili, utasalimiwa na mfanyikazi wa saikolojia ya jamii ambaye atakupa usaidizi na kuandamana nawe kwenye kipindi chote cha wewe kukaa nasi. Kila wiki, mtakutana kwa takribani dakika 45 na mfanyikazi huyo. Atajaribu kukusaidia katika kutimiza malengo ambayo wewe mwenyewe umetambua. Usaidizi huu unaweza kufikiwa kutokana na usikivu wa makini, usaidizi, maelezo, usaidizi wa taratibu na mapendekezo fulani kwa rasilimali nyingine zenye manufaa.

Ushuhuda wa mkazi: “Kupitia kwa Logifem, tunakusaidia na kukuonyesha namna maisha yalivyo mazuri, kwamba tuko hapa kusonga mbele, wala si kubaki kwa mambo ya nyuma na kwa matatizo tuliyopitia. Kama tupo hapa, ni jukumu letu kuyaweka matatizo hayo kando na kuyatatua moja baada ya jingine polepole, lakini kwa uhakika”.

 

Wapi?

Logifem ni makazi yanayopatikana katika eneo la kusini magharibi mwa Montreal karibu na kituo cha treni za haraka. Hatuwasiliani anwani yetu kwenye tovuti ili kuimarisha usalama wa makazi yetu. Sehemu halisi inawasilishwa kwa mwanamke pindi anapokubali kuwa mkazi.

 

Ni hatua gani zinazofuatwa ili kuishi hapo?

  1. Pigia simu Logifem nambari 514-939-3172. Tuko wazi saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki Kisha tutakualika katika kikao chetu cha maelezo kinachofuata. Kama utahitaji makazi mara moja, tutaweza pia kukuelekeza kwa rasilimali zinazofaa.
  2. Hudhuria kikao cha maelezo: Kama ungependa kuishi Logifem, njoo na ushiriki katika kikao cha maelezo, ambacho kwa kawaida kinakuwepo Jumanne alasiri, ili kupata kujua zaidi kuhusu huduma zinazotolewa. Wanawake walio na haja kuishi Logifem wataweza kujaza fomu ya ombi na kisha kuzungumzia hali yao na wafanyikazi wetu wa mapokezi.
  3. Endelea kuwasiliana: Baadaye, kundi la kufanya kazi litahakikisha kwamba Logifem ndiyo rasilimali inayofaa kwako. Inawezekana kwamba kuna kipindi cha kusubiri kabla ya chumba kupatikana (kipindi hicho kinaweza kuwa siku chache hadi miezi michache). Ni muhimu kutupigia simu kila wiki ili kuthibitisha haja yako. Wafanyikazi wa mapokezi watawasiliana na wewe wakati chumba kitapatikana na kuzungumza maelezo ya mwisho na wewe.

Urefu gani?

Unaweza kuishi katika makazi kwa hadi mwaka mmoja.

Tunazo nyumba za maghorofa pia ambazo, zinapopatikana, zinapewa wanawake ambao awali wameishi Logifem. Ada ya nyumba ni 25% ya mapato unayopata na wanawake wanaweza kuishi hapo hadi miaka mitatu. Lazima huwe na makazi ya kudumu au hadhi ya uraia na kutimiza mpangilio mwingine wa Ofisi ya Upangaji ya Manispaa ya Montreal ili kuweza kuishi ndani.

Kwa maswali yote

Usisite kutupigia simu na kuzungumza na mmojawapo wa wanaoshughulika kama unahitaji ufafanuzi au kama unayo maswali piga simu nambari 514-939-3172

Rasilimali nyingine zenye manufaa

Zifuatazo ni baadhi ya nambari za simu na tovuti ambazo zinaweza kuwa zenye manufaa kwako.

INFO SOCIAL 811
Info-Social 811 ni huduma ya ushauriano kupitia kwa simu ambayo ni bure na ya siri.

Dial 8-1-1, inajulikana kwa kuangazia malalamiko ya afya ya kimwili. Nambari hii pia inakuwezesha kufikia haraka mtaalamu katika shughuli za saikolojia ya jamii endapo una tatizo la saikolojia ya jamii. Huduma inapatikana saa 24 kwa siku, siku 365 kwa mwaka. Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya hali mbalimbali ambazo zinaweza kufanya ukapiga nambari Info-Social 811:

→ Unapitia hali inayokufanya kuhisi wasiwasi.
→ Una wasiwasi kuhusu mpendwa wako.
→ Unapitia ugumu katika familia yako au ndoa yako.
→ Unaomboleza.
→ Unayo maswali kuhusu hali au tabia nyingine zinazokupa wasiwasi.

Kituo cha Mapendekezo cha Greater Montreal (2-1-1)
Kituo cha Mapendekezo cha Greater Montreal ni aina fulani ya orodha ya huduma zote za jumuia na huduma za umma ndani ya Montreal. Unapiga simu bila malipo kwa kupiga nambari 2-1-1 au kutembelea tovuti yao ili kupata mashirika yanayoweza kukusaidia na ugumu wako. Huduma zinatolewa kwa Kifaransa na Kiingereza. https://www.211qc.ca/
DHULUMA YA KINYUMBANI YA SOS
Kama unapata vurugu kutoka kwa mwanandoa mwenzako

Piga simu SOS ya vurugu ya kinyumbani – 1 800 363-9010 au tembelea tovuti yao:

http://www.sosviolenceconjugale.ca/

Ngao ya Athena
Ngao ya Athena inakupa usaidizi wa kitaalamu, huduma za uingiliaji kati na kinga ambazo zinazoeleka kitamaduni na kilugha kwa mahitaji ya wanawake ambao wameathirika kutokana na vurugu ya kinyumbani na watoto wao, pamoja na wanachama wa jumuia za makabila na utamaduni. Huduma za lugha mbalimbali zinatolewa na wafanyikazi wa kitaalamu wa kijamii, wakisaidiwa na wasaidizi wa kitamaduni ambao wamepewa mafunzo kwa madhumuni haya katika ofisi zetu kule Laval na Montreal. Makazi yetu yanatoa huduma za makazi ya dharura 24/7 katika mazingira salama na saidizi kwa wanawake na watoto ambao wameathirika na vurugu ya kinyumbani.

Tovuti: Http://shieldofathena.com/ Nambari za simu: 1-877-274-8117
Nambari ya simu ya maelezo ya lugha mbalimbali inapatikana pia:

Nambari ya simu ya maelezo ya lugha mbalimbali kuhusu Ngao katika vurugu ya kinyumbani na rasilimali nyingine
514-270-2900 (Montreal)
450-688-2117 (Laval)

MAELEZO KUHUSU HAKI
Vipeperushi vya maelezo kuhusu usaidizi wa kisheria, usaidizi wa kijamii, elimu, familia, kazi, upangaji, afya, bima ya ajira, n.k vyote vinapatikana kwa

  • Kifaransa
  • Kiswahili
  • Kiarabu
  • Kichina Kilichorahisishwa
  • Krioli
  • Kihispaniola

Katika kiungo kifuatacho cha tovuti:

www.servicesjuridiques.org/documentation/depliants/

Mashirika ya jumuia yanayosaidia wahamiaji

Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya rasilimali za jumuia zinazosaidia wahamiaji:

Ahuntsic-Cartierville

Kituo cha Usaidizi wa Wageni (CANA) – (514) 382-0735
Kituo cha Usaidizi wa Jumuia za Wahamiaji wa Bordeaux-Cartierville (CACI) – (514) 856-3511
Nyumba ya CACI (Maison CACI) – (514) 856-3511
Huduma za Jumuia kwa Minajili ya Wakimbizi na Wahamiaji – (514) 387-4477
Chama cha Usaidizi wa Wahamiaji Mashariki ya Kati (SAIMOC) – (514) 332-4222

Anjou
Anjou Mshikamano Carrefour – (514) 355-4417
Côte-des-Neiges- Notre-Dame-de- Grâce

Muungano wa Kuwakaribisha na Kuwatangamana Wahamiaji (ALAC) – (514) 737-3642
Karibu katika Notre-Dame-de-Grâce: Kuwakaribisha wageni – (514) 561-5850
Femmes du monde à Côte-des-Neiges – (514) 735-9027
Uimarishaji wa Chama Kipya cha Utangamano (PROMIS) – (514) 345-1615
Ukalimani, Usaidizi na Huduma za Mapendekezo kwa Wahamiaji (SIARI) – (514) 738-4763

LaSalle
Karibu katika Kituo cha Wahamiaji na Wakimbizi wa Kusini Magahribi Montreal / Kituo cha PRISME (AIRSOM / PRISME) – (514) 364-0939
Mercier-Hochelaga-Maisonneuve
Ofisa wa Mapokezi wa Wageni (ALPA) – (514) 255-3900
Montréal-Nord
Kituo cha Jumuia ya Lugha Mbalimbali cha Montreal-Kaskazini – (514) 329-5044
Pierrefonds-Roxboro
Kituo cha Utangamano wa Huduma Mbalimbali cha West Island (CIMOI) – (514) 693-1000
Plateau-Mont-Royal

Kituo cha Jumuia ya Wanawake wa Asia Kusini (CCFSA) – (514) 528-8812
Maskani ya Ulimwenguni – (514) 903-9739
Hirondelle, Mapokezi ya Wahamiaji na Huduma ya Utangamano – (514) 281-2038

Rosemont- La Petite-Patrie

Chama cha Makabila Mbalimbali cha Utangamano wa Watu Walemavu wa Quebec (AMEIPHQ) – (514) 272-0680
Kituo cha Alpha Sainte-Anne (CASA) – (514) 278-3715
Kituo cha Usaidizi Nyanjani wa Kisheria na Mpangilio wa Kijamii kwa Wahamiaji (COPSI) – (514) 729-7098
Kicho cha N A Rive cha Montreal – (514) 278-2157
Mkusanyiko wa Wanawake Wahamiaji ndani ya‎ Quebec (CFIQ) – (514) 279-4246
Kamati ya Usaidizi wa Wakimbizi ‎(CAR) – (514) 272-6060
Wanamawasiliano, Mapokezi ya Ajira ya Utangamano – (514) 271-3533
Mtandao wa Uingiliaji Kati wa Watu Wanaopitia Vurugu ya Mpango ‎(RIVO) – (514) 282-0661
Elimu ya Montreal na Huduma Tangamani ya Tamaduni Mbalimbali ‎(SEIIM) – (514) 660-5908

Saint-Laurent
Kituo cha Jumuia cha Bon Courage katika Sehemu ya Benoit (CCBC) – (514) 744-0897
Kituo cha Mapokezi na Mapendekezo ya Kijamii na Kiuchumi kwa Wahamiaji (CARI St-Laurent) – (514) 748-2007
Saint-Léonard
Karibu kwa Wahamiaji kutoka East Montreal (AIEM) – (514) 723-4939
Sud-Ouest

Kamati ya Elimu ya Watu Wazima kuhusu Burgundy Mdogo na St-Henri (CÉDA) – (514) 596-4422
Kituo cha Kijamii cha Usaidizi wa Wahamiaji ‎(CSAI) – (514) 932-2953

Verdun
Ville-Marie

Wakimbizi Hatua ndani ya‎ Montreal (ARM) – (514) 935-7799
Rasilimali za Tamaduni Tofauti za Carrefour (CRIC) – (514) 525-2778
Kituo cha Afrika – (514) 843-4019
Kiini cha Utangamano wa Kazi kwa Wahamiaji (CITIM) – (514) 987-1759
Huduma ya Familia ya Kichina katika eneo la Greater Montreal (SFCGM) – (514) 861-5244

Villeray-Saint-Michel-Parc-Extension
Usaidizi wa Mawasiliano na Tamaduni Mbalimbali katika Carrefour (CLAM) – (514) 271-8207
Nyumba yaHaiti – (514) 326-3022
Mikono Midogo ‎(Petites-Mains) – (514) 738-8989